WAJASIRIAMALI WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA MIKOPO
Meneja Mahusiano wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Christabel Hiza kulia akitoa elimu kwa mkazi wa Jiji la Tanga Maulidi Omari wakati alipotembelea banda lao.
WAJASIRIAMALI nchini wametakiwa kuchangamkia fursa za mikopo zinazotolewa na Benki na NMB ili waweze kuimarisha biashara zao na hivyo kukuza kipato chao na jamii zinazowazunguka.
Hayo yalibainishwa na Meneja Mahusiano wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Christabel Hiza wakati akizungumza katika viwanja vya Tangamano mjini Tanga kunakoendelea maonyesho ya wiki ya vijana Taifa.
Alisema kwamba lengo lao la kushiriki kwenye maonyesho hayo ni kutoa elimu kwa wateja ambazo wamekuwa wakizitoa ikiwemo kufungua akaunti, kununua bidhaa na mikopo mbalimbali inayopatikana ili kuweza kuwasaidia kuweza kuwasaidia kwenye kukuza mitaji ya biashara zao.
“Vijana wakiweza kujiunga kwenye vikundi vidogo vidogo wanaweza kupewa elimu ya utawala bora ambayo itawawezesha kukopesheka hatua inakaayowasaidia kuweza kupata mitaji ya kuendesha shughuli zao za kujiingizia kipato “Alisema.
Hata hiyo alisema kwamba sambamba na hayo lakini pia wanatoa elimu na kuhamasisha kuhusu mpango wao mpya wa Kliki ambao unampa fursa mteja ambaye anajiunga nao kuweza kupata huduma za kibenki kiganjani.
No comments: