UHABA WA NAFASI CHANGAMOTO NAMBA MOJA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE

Mkurugenzi Mtendaji aeleza mikakati iliyopo kuondoa changamoto hiyo

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete(JKCI) Profesa Mohamed Janabi amesema pamoja na mafanikio makubwa ambayo wameyapata katika kipindi cha miaka mitatu ya uwepo wa taasisi changamoto namba kwao ni ufinyu wa nafasi.

Profesa Janab ambaye ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya moyo amesema uwepo wa taasisi hiyo imesaidia kuokoa mamia ya Watanzania ambao wamekuwa wakitibiwa hapo lakini akiulizwa changamoto inayowakabili ni nafasi.Ameeleza hayo wakati anazungumza na Michuz Blog kwenye mahojiano maalum yaliyofanyika ofisini kwake jijini Dar es Salaam ambapo ametumia nafasi hiyo kwa sehemu kubwa kuzungumzia mafanikio lakini pia amezungumzia changamoto.

"Nikiulizwa leo changamoto kubwa hapa kwetu ni nafasi.Kutokana na idadi kubwa ya wagonjwa wanaokuja hapa kwetu tumejikuta tunakabiliwa na uhaba wa nafasi." Bahati nzuri kuna mazungumzo yanaendelea ya kupatikana kwa jengo jingine ingawa hajafahamu litakuwa wapi.Tunaamini tukipata jengo jipya angalau tutaondoa hii changamoto iliyopo,"amesema Profess Janab.

Ameongeza mwishoni mwa mwaka huu kutakuwa na sherehe za miaka 50 za ushirikiano kati ya China na Tanzania, hivyo huenda wakaingia makubaliano maana tayari kuna mazungumzo yanaendelea ya kutusaidia kwenye ujenzi wa jengo jingine.

Amefafanua wagonjwa wa moyo wa huwezi kuwalaza chini hivyo kuna wakati mwingine hata upasuaji unasimama kutokana na ufinyu wa nafasi.Profesa Janab ametaja changamoto ya pili ni nyingine uhaba wa vifaa katika upasuaji mkubwa wa moyo kwani vifaa vyake vinatoka mbali na gharama yake ni kubwa.

Wakati changamoto ya tatu ni wananchi kutokuwa na ari ya kuchangia gharama za kutibu magonjwa ya moyo ambayo ni kubwa na ndio "Maana tunawashauri wananchi kuchangia.Kwa kuwa gharama ni kubwa tunawahamasisha wananchi kuwa na kadi ya bima ya afya," amefafanua.

Profesa Janab ametoa rai ya kuongezwa kwa watalaam wa upasuaji ili kwa siku za baadae kuwe na hospitali za aina hiyo ziwe kwenye kanda zote na hiyo itasaidia kunguza msongamano wa wagonjwa ndani ya taasisi hiyo.

No comments: