Shule ya Msingi ya Uzuri yapata Maktaba
Na Mwandishi wetu,
Wanafunzi nchini wametakiwa kujibidisha kusoma vitabu mbalimbali sio kwa malengo ya kufaulu mitihani pekee, bali pia kwa ajili kupata elimu na maarifa mapya yatakayowasaidia kukabiliana na changamoto za maisha.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr. Ntuyabaliwe Jacqueline Mengi ametoa wito huo jijini Dar es salaam wakati akizindua maktaba ya shule ya Msingi Uzuri, iliyopo Kata ya Manzese, Manispaa ya Ubungo, ambayo imekarabatiwa na kuwekwa vitabu kwa hisani ya taasisi hiyo.
Mkurugenzi huyo pia amewashawishi wanafunzi wa shule za msingi nchini wa kuanzia darasa la nne hadi la saba kushiriki shindano la Andika Challenge la kuandika na kubuni hadith zenye mafundisho, lililoanzishwa na Taasisi hiyo, na kuwahakikishia kuwa kila mkoa utatoa washindi.
Wakizungumza katika hafla hiyo Afisa Elimu wa Manispaa ya Ubungo Chausiku Masegenya, na Mwenyekiti wa Kamati ya shule Bw. Yassin Shaaban Bakari wameipongeza Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe kwa ufadhili huo unaounga mkono jitihada za serikali za kuboresha utoaji wa elimu nchini.
Aidha Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Bw. Sifuni Mbwambo na Mwanafunzi Vivian Herbeth wameipongeza taasisi ya Dr Ntuyabaliwe na kusisitiza kuwa shule hiyo ina maendeleo mazuri kitaalum ingawa inakabiliwa na changamoto mbalimbali, zikiwemo upungufu wa samani hasa kwa walimu, uchakavu wa majengo, na ukosefu wa uzio.
Mgeni rasmi Afisa Elimu wa Manispaa ya Ubungo Chausiku Masegenya akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuzindua maktaba iliyokarabatiwa na kuwekwa vitabu kwa hisani ya taasisi ya Dr. Ntuyabaliwe katika shule hiyo, iliyopo Kata ya Manzese, Manispaa ya Ubungo jana jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr. Ntuyabaliwe Jacqueline Mengi (kushoto) akizungumza na wanafunzi pamoja na walimu wa shule ya Msingi Uzuri (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kuzindua maktaba iliyokarabatiwa na kuwekwa vitabu kwa hisani ya taasisi ya Dr. Ntuyabaliwe katika shule hiyo, iliyopo Kata ya Manzese, Manispaa ya Ubungo jana jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Uzuri, Bw. Sifuni Mbwambo na kulia ni Mratibu wa Elimu kata ya Manzese, Laura Tesha.
Baadhi ya wawakilishi wa wanafunzi wa shule ya msingi Uzuri wakimsikiliza Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr. Ntuyabaliwe Jacqueline Mengi (hayupo pichani) wakati wa hafla fupi ya kuzindua maktaba iliyokarabatiwa na kuwekwa vitabu kwa hisani ya taasisi ya Dr. Ntuyabaliwe katika shule hiyo, iliyopo Kata ya Manzese, Manispaa ya Ubungo jana jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya shule Bw. Yassin Shaaban Bakari akitoa neno la shukrani kwa taasisi ya Dr. Ntuyabaliwe kwa kukarabati jengo la maktaba pamoja na kuweka vitabu wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa maktaba hiyo iliyofanyika katika shule hiyo, iliyopo Kata ya Manzese, Manispaa ya Ubungo jana jijini Dar es Salaam.
Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Uzuri, Bw. Sifuni Mbwambo, Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr. Ntuyabaliwe Jacqueline Mengi pamoja na Mratibu wa Elimu kata ya Manzese, Laura Tesha wakitazama picha za maktaba ilivyokuwa hapo awali kabla ya kufanyiwa ukarabati na taasisi ya Dr. Ntuyabaliwe wakati wa hafla ya kuzindua jengo la maktaba hiyo iliyofanyika katika shule hiyo, iliyopo Kata ya Manzese, Manispaa ya Ubungo jana jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr. Ntuyabaliwe Jacqueline Mengi akikata utepe kuzindua eneo la maktaba iliyokarabatiwa na kuwekwa vitabu kwa hisani ya taasisi ya Dr. Ntuyabaliwe katika shule hiyo, iliyopo Kata ya Manzese, Manispaa ya Ubungo jana jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Uzuri, Bw. Sifuni Mbwambo (kulia), Mwenyekiti wa Kamati ya shule Bw. Yassin Shaaban Bakari (katikati), Mratibu wa Elimu kata ya Manzese, Laura Tesha (kushoto) pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wakiwakilisha wenzao.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr. Ntuyabaliwe Jacqueline Mengi na Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Uzuri, Bw. Sifuni Mbwambo wakifunua pazia kwenye kibao maalum cha wafadhili ambao ni taasisi ya Dr. Ntuyabaliwe waliohusika kukarabati na kuweka vitabu kwenye jengo la maktaba hiyo shuleni hapo wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa maktaba hiyo iliyofanyika katika shule hiyo, iliyopo Kata ya Manzese, Manispaa ya Ubungo jana jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia ni Mwenyekiti wa Kamati ya shule Bw. Yassin Shaaban Bakari (kulia).
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
No comments: