P DIDDY ATARAJIA KUITWA BABA TENA

Related image

Sean ‘Diddy’ Combs na Cassie

LICHA ya kuwa na watoto wengi mithili ya timu ya mpira wa kikapu, rapa mkongwe kwenye Muziki wa Hip Hop, P Diddy anatarajia kuitwa baba kutoka kwa mchumba wake, Cassie.

Katika picha mbalimbali zilizosambaa juzikati, zilikuwa zikimuonesha Cassie akiongozana na P Diddy huku kitumbo kikiwa ‘ndi’. Endapo Cassie atajifungua salama, atakuwa mtoto wake wa kwanza kuzaa na rapa huyo ambaye kwa sasa ana watoto sita aliozaa na wanawake tofauti. Katika mahojiano aliyowahi kufanya hivi karibuni, P Diddy alikaririwa akisema; “Nawapenda watoto wangu, naelekea watoto nane sasa bila kuwa na tatizo.”

The post P DIDDY ATARAJIA KUITWA BABA TENA appeared first on Global Publishers.

No comments: