MWILI WA PANCHO LATINO WAAGWA DAR, KUZIKWA GAIRO

MASTAA, wadau wa sanaa ya muziki na waombolezaji mbalimbali wamejitokeza leo Ijumaa, Oktoba 12, 2018, kuaga mwili wa aliyekuwa Producer wa Studio za H-Bits, Pancho Latino, katika Hospitali ya Lugalo jijini Dar.

Pancho maarufu kama Mafia, alifariki dunia juzi jioni kwenye ajali ya kuzama na maji wakati akiogelea kwenye Kisiwa cha Mbudya jijini Dar es Salaam.

Mwili wa marehemu umeagwa leo Dar na katika ibada maalum ya kuaga na utasafirishwa kwenda nyumbani kwao Gairo, mkoani Morogoro kwa ajili ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika kesho Jumamosi.

The post MWILI WA PANCHO LATINO WAAGWA DAR, KUZIKWA GAIRO appeared first on Global Publishers.

No comments: