Sitaki Kutumika Kwenye Kampeni 2020, Niliona Madhara Yake- Ray
Muigizaji wa Bongo movie Vicent Kigosi maarufu kama Ray amefunguka na kuweka wazi kuwa hataki tena kutumiwa na Vyombo vya siasa Kwenye kampeni za uchaguzi.
Ray amefunguka na kusema anaunga Mkono Kauli na Katibu kuwa hawataki kutumia tena wasanii Kwenye kampeni za siasa kwani na yeye ameona madhara ya kutumika Kwenye kampeni hizo.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Millard Ayo Ya, Ray amefunguka zaidi na kusema
Kimsingi yeye alichozungumza Katibu mimi siwezi kukataa alichozungumza cha muhimu tusubiri tuone kama kweli wasanii hawatotumika kwa ajili ya kampeni lakini mimi binafsi sitaki wanaitumie kwa sababu nimeona madhara ya kutumika Kwenye kampeni lakini dunia nzima hata Marekani tunaona wakina Trump wanatumia wasanii kufanya kampeni lakini kama Katibu Bashiru kazungumza basi atakuwa ana target kwaiyo naheshimu maamuzi yake lakini kama wakitumia wasanii basi tutawasuta kwa Kauli waliyotoa”.
Wasanii wengi waliotumika kupiga kampeni 2015 walikosolewa sana kutokana na baadhi yao kuhama hama vyama kwa maslahi yao binafsi ya kujiingizia kipato.
The post Sitaki Kutumika Kwenye Kampeni 2020, Niliona Madhara Yake- Ray appeared first on Ghafla!Tanzania.
No comments: