Nandy Atangaza Ndoa na Mpenzi Wake Mpya

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Faustina Charles ‘Nandy’ amefunguka na kusema hivi sasa amepata mpenzi mpya na endapo Mungu atajaalia basi ndoa itafungwa hivi karibuni.

Kwenye mahojiano na Risasi Vibes, Nandy amesema kwamba kwa sasa hana ukaribu wa aina yoyote ile na msanii mwenzake, William Lyimo ‘Billnas’ ambaye pia amewahi kuwa mpenzi wake, baada ya matatizo yaliyowahi kutokea ya kuvuja kwa video yao chafu.

Nandy amesema kwa sasa hivi amepata mpenzi mwingine na kama Mungu akijalia, hivi karibuni atafunga ndoa.

Shemeji yenu yupo, tusubiri ndoa tu kama Mungu akijalia lakini siwezi  kutaja ni lini kwa sababu naweza nikataja halafu isifanyike, kwa hiyo sasa hivi namuomba tu Mungu iweze kutimia”.

Nandy amefunguka pia kuwa kwa sasa hana urafiki wowote na Billnas tangu sakata lao la video chafu lakini wakikutana wanapiga stori kawaida tu.

The post Nandy Atangaza Ndoa na Mpenzi Wake Mpya appeared first on Ghafla!Tanzania.

No comments: