Nafurahi Kuona Wasanii wa Kike Tukiwa na Ushindani.
Msanii wa kike kwenye anga za bongo fleva Nandy amefunguka na kusema kuwa amekuwa akifurahishwa sana na kasi ya wasanii wenzake wa kike kwa sasa kutokana na kuwa na ushindani sana sio kama hapo mwanzo walivyokuwa wakisemwa kuwa wasanii wa kike wamekuwa wakibweteka.
Nandy anasema kuwa tofauti na ilivyokuwa hapo awali kuwa katika muziki kulikuwa kumetawaliwa na wanaume tu, sasa hivi kuna ongezeko kuba la wasanii wa kike na kumekuwa na ushindani sana kitu kinachotoa matumaini kuwa wanawake wameamka na kutambua kuwa hata wao wanaweza.
Nafurahi sana kuona wasanii wa kike wakishindana vipaji na wanaume katika muziki ,kwangu nifaraja kubwa na kama tutaendelea hivi basi tutafika mbali.
The post Nafurahi Kuona Wasanii wa Kike Tukiwa na Ushindani. appeared first on Ghafla!Tanzania.
No comments: