DC SOPHIA KIZIGO AAHIDI KUSHIRIKIANA NA WANANCHI WA MGOMBASI KUBORESHA SHULE YA MKUYUNI
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii
MKUU wa Wilaya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Mfaume Kizigo amefanya ziara katika Kata ya Mgombasi ambapo amepata nafasi ya kutembelea ya Shule ya Msingi Mkuyuni.
Shule awali ilikuwa ya nyasi tu na moja ya mkakati wa Mkuu wa Wilaya ni kuendelea kuboresha mazingira ya shule hiyo.
Akizungumzia shule hiyo Kiziga amesema wananchi kwa nguvu zao walijitolea wakajenga madarasa." Hivi sasa kuna madarasa matano ambayo yapo kwenye hatua nzuri,"amesema Mkuu wa Wilaya .
Pia amesema kwa kuwa kuna uhaba wa vyumba viwili vya madarasa na hakuna kabisa shule ya awali (chekechea), wanafunzi wa chekechea, darasa la kwanza na la pili wanasomea katika chumba kimoja cha darasa.
Amefafanua wamekubaliana na wananchi wa hapo kwamba wajenge hayo madarasa mawili mpaka boma, kisha Serikali watachangia vifaa vya viwandani.
Mkuu wa Wilaya Sohia Kizigo akimtazama Mmoja wa Wanafunzi aitwaye Zamda akiandika ubaoni kujibu maswali ya hesabu aliyoandikiwa na Mkuu wa Wilaya kujiridhisha kama bado kanuni ya KKK inawasaidia na inawafanya waelewe vizuri
Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo,Mh Sophia Kizigo akikabidhiwa taarifa ya shule na Mwalimu mkuu wa shule ya Makuyuni
Mkuu wa Wilaya Mh Kizigo pamoja na ujumbe wake wakikagua moja ya darasa ambalo Wanafunzi wanasoma madarasa 3 kwa wakati mmoja,kutoka na shule hiyo kuwa na uhaba wa madarasa.
No comments: