MBEZI JUU YAIFURAHIA MERIDIANBET KWA KUWAKUMBUKA

 


MBEZI Juu iliyopo jijini Dar-es-salaam leo imefurahia kufikiwa na mabingwa wamichezo ya kubashiri kampuni ya Meridianbet ambao wamefika eneo hilo mapema leo kwajili ya kuhakikisha wanatoa msaada.

Kurudisha kwenye jamii iliyowazunguka ndio umekua utaratibu wa Meridianbet haswa kwa wale wenye uhitaji, Ambapo leo kampuni hiyo iliamua kufika katika hospitali ya Ndumbwi Mbezi Juu na kutoa msaada wa vifaa vya usafi ambavyo vitasaidia kuimarisha usafi eneo hilo.

Hospitali ya Ndumbwi kwa mara ya kwanza inapokea msaada wa vifaa vya usafi kutoka kwa mabingwa wa michezo ya kubashiri mapema, Huku wakionesha kufurahishwa na jambo hilo lililofanywa na kampuni ya Meridianbet.

Bado mabingwa wa michezo ya kubashiri Meridianbet wanaendelea kuhakikisha unapigwa mkwanja wa kutosha kupitia michezo mbalimbali inayopigwa haswa michuano ya ligi ya mabingwa ulaya inayopigwa katikati ya wiki hii ambapo wanaendelea kumwaga ODDS BOMBA kila siku.

Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Masoko ndani ya Meridianbet Bi Nancy Ingram alipata nafasi ya kuzungumza machache katika hafla hiyo "Tunatambua umuhimu wa usafi wa mazingira maana usafi ni afya ndio maana leo tumeweza kuleta vifaa hivi katika hospitali hii kwa dhumuni la kuimarisha usafi katika mazingira ya hospitali na kuondokana na magonjwa yatokanayo na uchafu".

Aidha Diwani wa eneo la Mbezi Juu Bi Anna Lukindo ambaye alikuepo kwenye tukio hilo alipata nafasi ya kuzungumza machache juu ya jambo hilo la kiungwana lililofanyika “Kiukweli nipende kuwashukuru Meridianbet kwa kufika katika hospitali yetu ya Ndumbwi na kuweza kutoa vifaa vya usafi ambavyo vitasaidia kuhakikisha mazingira ya hospitali yetu yanakua makazi, Niwape pongezi kwa jambo hilo wasiishie hapa tu waendelee kuwashika mkono na wengine”

No comments: