Trump Akana Shutuma Dhidi Yake Kuwa Yeye ni Mbaguzi

Rais wa Marekani, Donald Trump amesisitiza kuwa yeye si mbaguzi baada ya mashambulizi yake kupitia Twitter dhidi ya wabunge wanne wanawake kukemewa vikali.

 

Katika ukurasa wa Twitter aliwataka wanawake hao wasio na asili ya Marekani, ”kuondoka” kuelekea kwenye nchi zao walipotoka.

Kitendo hicho kiliamsha ghadhabu, alikataa shutuma kuwa yeye ni mbaguzi: ”sina asili ya ubaguzi mwilini mwangu!”.

 

Bunge la wawakilishi linajiandaa kupigia kura makubaliano ya pamoja ya kukemea kauli zake, huku hatua hiyo ikitegemewa kupita kutokana na kuwepo wawakilishi wengi wa Democrats.

Awali, wabunge Alexandria Ocasio-Cortez, Ilhan Omar, Ayanna Pressley na Rashida Tlaib walitangaza kupuuza matamshi ya Trump wakidai yanalenga kuwaondoa kwenye mstari.

 

Wabunge hao waliwataka watu nchini humo kupuuza maneno yake. Rais Trump hakutamka majina ya wanawake hayo kwenye ukurasa wa Twitter, lakini yaliyokuwemo kwenye matamshi yake yalionesha wazi kuwepo kwa uhusiano na wabunge hao.

 

Alisababisha hasira baada ya kusema wanawake ”ambao asili yao wanatoka kwenye nchi ambazo serikali zake ni zina machafuko” warejee makwao.

 

Wakizungumza na waandishi wa habari wanawake hao wamesema, hivi sasa watu waweke akili zao kwenye sera za nchini Marekani na si maneno ya raisi Trump.

Bi Pressley amezitupilia mbali jitihada za raisi ”kutukandamiza na kutunyamazisha”, akiongeza kuwa walikuwa ”zaidi ya watu wanne.”

 

”Kikosi chetu ni kikubwa.Kikosi chetu kinahusisha mtu yeyote aliye tayari kujenga ulimwengu wa usawa na haki,” alisema.

 

Wanawake wote wanne wamesisitiza kuwa huduma za afya, matumizi mabaya ya silaha, pia kushikiliwa kwa wahamiaji katika mpaka kati ya Marekani na Mexico ni masuala ya kutazamwa.

 

Bi Omar amesema maneno ya Trump yanadhihirisha kuwa ”mashambulizi ya ubaguzi wa rangi” dhidi ya wanawake wanne maneno ambayo ”hayana maana yeyote isipokuwa kuigawanya nchi yetu”.

 

Awali raisi alisema kwa bi Omar alikuwa akiunga mkono kundi la wanamgambo za al-Qaenda. ”Ninajua kuwa kila muislamu aliyeishi nchini humu na duniani kote amesikia kuhusu kauli hiyo hivyo sitaipa nafasi kwa kuijibu,”.aliongeza kuwa hakutegemea jumuia ya watu weupe kujibu baada ya mtu mweupe ”kuua kwenye shule au jumba la sinema, msikiti au sinagogi”.

 

Bi Ocasio-Cortez alisimulia kuhusu alipotembelea Washington DC akiwa mtoto, akisema watu wawaambie watoto wao kuwa ”chochote kile atakachosema raisi, nchi hii ni yenu”.

 

Mgogoro umeanzaje?

Siku ya Ijumaa, Bi Ocasio-Cortez, Bi Tlaib na Bi Pressley alitoa ushuhuda mbele ya wabunge kuhusu hali za wahamiaji wanaoshikiliwa kwenye vituo ambavyo walivitembelea.

 

Wabunge wa Democrat kwa kiasi kikubwa wameushutumu utawala wa Trump hasa namna anavyodhibiti mpaka, wakisema wanawashikilia wahamiaji ambao sasa wana hali mbaya.

 

Trump amewatetea maafisa wake mpakani .Utawala wake ulitangaza sheria mpya inayoanza kutumika tarehe 16 mwezi Julai, sheria inayokataa kutoa hifadhi kwa mtu yeyote anayevuka mpaka wa kusini ambaye hajaomba kupatiwa hifadhi kwenye ”nchi ya tatu”.

 

Wabunge wa Democraticna Republican wamesemaje?

Wana Democrat wamekemea vikali kauli ya Trump, na wengi kwa haraka walisema ni shambulio la kibaguzi.

Viongozi wa Republican hata hivyo hawajazungumza sana. Seneta Mitch McConnell amesema atajibu maswali siku ya Jumanne.

Waziri wa fedha Steven Mnuchin amesema: ”sioni kama matamshi hayo ni ya kibaguzi, raisi amefafanua kauli yake.” kisha akabadili mada.

Seneta na aliyewahi kuwania uraisi Mitt Romney amesema kauli za Trump ”zinaharibu, kukandamiza na kugawanya watu”.

The post Trump Akana Shutuma Dhidi Yake Kuwa Yeye ni Mbaguzi appeared first on Global Publishers.

No comments: